• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yaimarisha hatua za kiusalama kwa ajili ya sikukuu ya Eid-el-Kabir

    (GMT+08:00) 2017-09-01 09:08:29

    Idara ya usalama ya Nigeria imeimarisha hatua za usalama dhidi ya tishio la shambulizi la kigaidi katika sikukuu ya Eid-el-Kabir.

    Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa tarehe mosi na nne mwezi huu ni siku za mapumziko kwa ajili ya sherehe hiyo.

    Msaidizi wa kamanda mkuu wa Polisi Bw Salisu Fagge amethibitisha kuwa hatua za usalama kwa ajili ya sikukuu hiyo zimeimarishwa. Makamishna watatu wa polisi kutoka mji mkuu, majimbo ya Niger na Kaduna wamefanya maandalizi ya kuhakikisha usalama katika kipindi cha sikukuu hiyo.

    Polisi wataongeza doria kwenye barabara kutoka Abuja hadi Kaduna, na kuwahakikishia madereva kuwa hatua za usalama zinazochukuliwa zitaweza kukabiliana na tishio lolote.

    Kamanda mkuu wa vikosi vya usalama na ulinzi wa Nigeria Bw Abdullahi Muhammad amesema polisi elfu 40 na wabwa wa polisi wamepangwa kote nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako