• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Russia azungumzia ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika siku za baadaye

    (GMT+08:00) 2017-09-01 09:21:14

    Wakati Mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS unakaribia, rais Vladimir Putin wa Russia ametoa makala akieleza maoni yake kuhusu ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika siku za baadaye.

    Kwenye makala hiyo iitwayo "nchi za BRICS---kufungua upeo mpya wa macho kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati", rais Putin amesema China ikiwa mwenyeji wa mkutano huo, inauwezesha ushirikiano kati ya nchi za BRICS kupata maendeleo muhimu ya pamoja katika sekta za siasa, uchumi na utamaduni, na hadhi ya nchi hizo duniani pia imeinuka kidhahiri.

    Pia amesisitiza lengo la ushirikiano wa kiujenzi kati ya nchi za BRICS ni kuanzisha utaratibu wa usawa, na kutoa fursa zenye usawa kwa nchi mbalimbali duniani. Amependekeza nchi za BRICS kutekeleza sera za karibu zaidi za kidiplomasia hususan katika Umoja wa Mataifa, kundi la nchi 20 pamoja na mashirika mengine ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako