• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Tajikistan

    (GMT+08:00) 2017-09-01 09:49:03

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Tajikistan Bw Emomali Rakhmonov ambaye yuko ziarani nchini China, na kuhudhuria mazungumzo ya nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea.

    Viongozi hao wawili wamekubaliana kujenga uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China na Tajikistan, ili kutimiza maendeleo makubwa katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China inapongeza Tajikistan kuunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Pande hizo mbili zitahimiza kuunganisha pendekezo hilo na mkakati wa maendeleo ya taifa ya Tajikistan kabla ya mwaka 2030, na kutekeleza mipango ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kwenye ujenzi wa miundombinu, nishati, bandari na mtandao wa internet.

    Baada ya mkutano huo, viongozi hao wamesaini na kutoa taarifa ya pamoja kuhusu kujenga uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Tajikistan, na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano zaidi ya kumi ya ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako