• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 68 wa kundi la IS wauawa katika mashambulizi ya anga nchini Iraq

    (GMT+08:00) 2017-09-01 18:16:32

    Wapiganaji 68 wa kundi la kigaidi la IS wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Iraq katika jimbo la Anbar, nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya jeshi la Iraq imesema, shambulizi dhidi ya mji wa al-Qaim limeharibu ghala la silaha na moja ya makao makuu ya kundi hilo, huku shambulizi lingine katika mji wa Aana likiangamiza kambi moja ambamo wapiganaji wa kundi hilo walijificha.

    Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza kuwa, jeshi la serikali limeliondoa kundi la IS katika mji wa Tal Afar, na kwamba jimbo la Nineveh kwa sasa linadhibitiwa tena na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako