• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wazihimiza nchi zinazoibuka kiuchumi kuathiri dunia kwa maendeleo yao

    (GMT+08:00) 2017-09-01 18:46:28

    Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo UNDP Bw. Achim Steiner amesema nchi za BRICS zinajadili masuala ya kikanda na kimataifa kwa mujibu wa uzoefu wa maendeleo, jambo hili linaonesha kwamba nchi zinazoibuka kiuchumi zinaweza kuiathiri dunia kwa maendeleo yao.

    Bw. Steiner amesema nchi hizo zimepata njia mwafaka ya kujiendeleza kiuchumi hatua kwa hatua baada ya maendeleo ya miaka kumi iliyopita, na zimepata jukwaa la kufanya mawasiliano na ushirikiano ambalo ni utaratibu wa BRICS. Amesema Umoja wa Mataifa unatarajia kuwa si kama tu nchi hizo zitapata maendeleo halisi kwenye mambo ya uchumi na jamii, bali pia zitatoa mchango kwa maendeleo ya dunia, na kushirikiana katika kukabiliana na chamgamoto za binadamu wote zikiwemo mazingira, umasikini na amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako