• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaipongeza Iran kwa kutekeleza makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyulia

    (GMT+08:00) 2017-09-01 19:16:38

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema China inaipongeza Iran kwa kutekeleza makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia la Iran, na kutoa pongezi kwa juhudi za Iran na Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa IAEA kwa kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Bi Hua alikuwa akijibu swali kuhusu ripoti ya mkurugenzi wa IAEA inayothibitisha kwamba Iran imetekeleza makubaliano hayo. Amesema China inatarajia pande husika zitaendelea kutekeleza makubaliano hayo kwa makini, na IAEA itaendelea kutekeleza wajibu kwa msimamo wenye usawa na wa kitaaluma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako