• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakabiliana na uchafuzi wa hewa katika sehemu ya kaskazini

  (GMT+08:00) 2017-09-01 19:24:54

  Wizara ya uhifadhi wa mzingira ya China leo imeanza operesheni ya kushughulikia uchafuzi wa mazingira katika sehemu za Beijing, Tianjin, Hebei na nyingine jirani, ili kuboresha hewa katika majira ya baridi ya mwaka huu.

  Katika miaka ya hivi karibuni, uchafuzi wa hewa umepungua katika sehemu za Beijing, Tianjin, Hebei na miji mingine jirani, hata hivyo wakati wa majira ya baridi uchafuzi wa hewa bado unatokea mara kwa mara katika sehemu hizo. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa mazingira ya hewa iliyoko chini ya wizara ya uhifadhi wa mazingira ya China Bw. Liu Bingjiang amesema, ili kukabiliana na changamoto hii, wizara hiyo imeagiza wataalam na idara zinazohusika kufanya utafiti kwa makini. Anasema,

  "Mwaka huu kwa mara ya kwanza tumeweka vigezo vya kupunguza uchafuzi wa hewa, yaani kwa jumla tutapunguza kiwango cha vumbi zenye ukubwa chini ya mikoroni 2.5 ( PM2.5 ) na siku zenye uchafuzi mkubwa kwa asilimia 15 katika siku za baridi. Lakini malengo ya miji mbalimbali yana tofauti ndogo, na kila sehemu imepewa vigezo maalumu kutokana na hali tofauti."

  Ili kutimiza malengo hayo, wizara ya uhifadhi wa mazingira imetoa hatua nyingi zinazohusu matumizi ya makaa ya mawe, viwanda, magari, vitendo vya kurusha vumbi, na mbinu za kukabiliana na hali mbaya ya uchafuzi. Aidha wizara hiyo pia itaratibu ushirikiano kati ya idara zinazohusika, kuimarisha usimamizi na ukaguzi, kutoa uungaji mkono kupitia sera ya uchumi, kusukuma mbele utafiti wa sayansi na kudadisi majukumu, ili kuhakikisha hatua za kushughulikia uchafuzi wa hewa zinatekelezwa vizuri.

  Bw. Liu Bingjiang amesema, kiwango cha uchafuzi wa hewa kinatokana na utoaji wa uchafu na hali ya hewa. Malengo ya mwaka huu ya kupunguza utoaji wa uchafu ni magumu kuliko mwaka jana, lakini anaamini yatatimizwa. Anasema,

  "Kazi za mwaka huu ni karibu mara tatu kuliko mwaka jana. Mwaka jana tulizisadia familia laki nane kutumia umeme na gesi badala ya makaa ya mawe, na mwaka huu, idadi hii itakuwa milioni tatu. Mwaka jana tulifunga vinu vidogo karibu elfu 10 vya kutumia makaa ya mawe, na mwaka huu tutafunga elfu 44. Hivyo kama hali ya hewa itakuwa nzuri, tutakuwa na hewa bora."

  Aidha mwaka huu wizara ya uhifadhi wa mazingira pia imefikia makubaliano na miji ya Beijing na Tianjin, na mikoa ya Hebei, Shanxi, Shandong na Henan kuhusu majukumu ya uchafuzi, na kama malengo ya kupunguza uchafuzi hayatatimizwa, maofisa wanaohusika watawajibishwa. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa juhudi za kuhifadhi mazingira ya China Bw. Liu Changgen anasema,

  "Tutafuatilia zaidi utekelezaji wa hatua za kuhifadhi mazingira, na kuwawajibisha maofisa wanaohusika. Hivi sasa na wakati wa siku za baridi, hatutavumilia vitendo vya kupuuza juhudi za kukinga uchafuzi wa hewa katika sehemu za Beijing, Tianjin, Hebei na nyingine jirani."

  Habari zinasema wizara ya uhifadhi wa mazingira itafanya ukaguzi kwa duru 15, unaolengea kuzihimiza idara zinazohusika kutekeleza mpango wa operesheni ya kukinga uchafuzi wa hewa kwa makini, na kuongeza nguvu ya kupambana na vitendo haramu vya kutoa uchafu, ili kuboresha hewa katika siku za baridi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako