• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na Afrika Kusini zashirikiana kupiga jeki sekta ya utalii ya Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-09-01 20:05:56

    Kampuni ya Rwanda imefanya makubaliano na kampuni ya Afrika kusini itakayofanikisha juhudi za nchi hiyo kupiga jeki sekta ya utalii nchini humo. Kwa mujibu wa kampuni ya kuandaa mikutano ya Ikaze iliyoko Rwanda, kampuni ya Crystal Events Africa ya Afrika Kusini ambayo pia inajihusisha na shughuli za kuandaa mikutano itaiuza Rwanda kwa wawekezaji pamoja na raia wa Afrika Kusini kuhusu uwezo wake wa kufanya mikutano kwa njia iliyo salama. Kampuni hiyo pia itatoa maelezo kuhusu vivutio vya utalii vya Rwanda kwa raia wa nchi hiyo. Makubaliano hayo yanakuja wakati ambapo bodi ya maendeleo ya Rwanda imetoa ripoti inayoonyesha kuwa jumla ya mapato yatokanayo na mikutano pamoja na maonesho ya kimataifa mwaka huu yaliongezeka na kufikia dola milioni 64 ikiwa ni juu ikilinganishwa na dola milioni 47 yaliyopatikana mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako