• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Misri zaalikwa mkutano wa BRICS China

    (GMT+08:00) 2017-09-01 20:06:43

    China imezialika Kenya na Misri kuhudhuria mkutano wa BRICS utakaofanyika mjini Xiamen.

    Nchi nyingine zilizoalikwa kwa mkutano huo ni pamoja na Tajikistan, Mexico na Thailand .

    Mkutano huo utaanza Septemba 3 hadi 5 ukijulikana kama BRICS Plus kutokana na kualikwa kwa nchi ambao sio wanachama.

    Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi amesema nchi hizo zimealikwa ili kupanua mjadala wa ushirikiano na kibiashara.

    Nchi wananchama wa BRICS ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kuisni.

    BRICS ilianzishwa mwaka 2011 kwa lengo la kuunganisha nguvu za kiuchumi na kuongeza sauti kwenye jukwaa la kimatafifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako