• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake Uganda wapinga masharti ya kupata mikopo

    (GMT+08:00) 2017-09-01 20:06:57

    Mashirika ya kijamii pamoja na wafanya biashara wanawake nchini Uganda wamepinga masharti magumu yanayowekwa na hazina ya kuwawezesha kina mama nchini humo. Kwa mujibu wa hazina ya kuwawezesha wanawake nchini Uganda, wafanya biashara wa kike wanatakiwa kujiweka kivikundi kabla ya kupatiwa mikopo.

    Jumla ya shilingi bilioni 43 zilitengwa na serikali ya Uganda lakini hadi kufikia sasa ni bilioni 21.5 tu ambazo zimetolewa na wizara ya fedha ya nchi hiyo.

    Akizungumza na radio China Kimataifa, katibu mkuu mtendaji wa chama cha maendeleo ya wanawake nchini humo UWONET Rita Aciro Lakor amesema tayari wamepokea malalamiko kutoka kwa wanawake kutoa kwa maeneo mbali mbali wakipinga masharti magumu yanayowekwa wanapokwenda kuomba fedha hizo.

    Wanawake hao wanadai kuwa kila mmoja wao ana malengo tofauti hivyo ni vigumu kufanya biashara kikundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako