• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhuru Kenyatta apokea hukumu ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-02 18:09:25
    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana amesema hakubali uamuzi wa mahakama ya juu ya kubatilisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu, lakini anaiheshimu hukumu hiyo, na atajitayarisha kugombea uchaguzi wa duru jipya.

    Uhuru kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, hukumu ya mahakama ya juu ni ya kisiasa, ushindi wake ni nia ya wananchi wa kenya. Amesema yupo tayari kushiriki kwenye uchaguzi wa duru jipya, na atapata uungaji mkono tena na wakenya. Uhuru pia amewataka wakenya wadumishe aman

    Wakati huohuo, Umoja wa Afrika pia umewahimiza watu wa Kenya waheshimu hukumu hiyo, na kudumisha hali ya utulivu.

    Uhuru alipata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti kwa kupata kura asilimia 54.27. Mshindani wake Raila Odinga kutoka kundi la upinzani NASA alikataa kupokea matokeo hayo, na kuifikisha kesi mahakama ya juu, ambayo ilitangaza kubatilisha matokeo hayo, na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike ndani ya siku 60.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako