• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa FAO aonya kuhusu kuongezeka kwa njaa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-02 18:10:09

    Mkurugenzi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa Jose Graziano da Silva ameonya kuwa, njaa inaongezeka barani Afrika kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame wa muda mrefu, mafuriko na migogoro.

    Graziano da Silva amesema hayo wakati akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Uganda ambapo alifanya mazungumzo na waziri wa kilimo, mifugo, viwanda na uvuvi wa Uganda bwana Vincent Bamulangaki Sempijja kuhusu kuendeleza kilimo endelevu na ushirikiano zaidi wa kimkakati kwa nchi isiyo na njaa.

    Naye bwana Sempijja ameeleza kuwa ingawa Uganda bado haijawa na hali ya wasiwasi ya chakula, lakini ilikabiliwa na wadudu walioshambulia na kuharibu mazao hasa mahindi na kuongeza kuwa uhamiaji wa wakimbizi kutoka Sudan Kusini kumeleta shinikizo zaidi la uhaba wa chakula.

    Tangu mapigano yalipotokea Sudan Kusini mwishoni mwa mwaka 2013, wakimbizi zaidi ya milioni moja wamevuka na kuingia Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako