• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini ina matumaini makubwa juu ya Mkutano wa BRICS

    (GMT+08:00) 2017-09-02 18:10:47

    Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema mkutano wa BRICS utakaofanyika mjini Xiamen China utatoa fursa ya kusaidia kufikia malengo ya maendeleo ya nchi za kusini.

    Akizungumza wakati akiondoka nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 9 wa wakuu wa nchi za BRICS unaoanza Septemba 3 hadi 9, Bwana Zuma amesema ushiriki wake katika mkutano huo utasaidia Afrika Kusini kupata mbinu mpya ya kukabiliana na changamoto tatu za umasikini, ukosefu wa ajira na ukosefu wa usawa.

    Afrika Kusini inatarajia majadiliano ya mkutano huo yatatafakari ushirikiano na kuunganisha mataifa kwa kuzingatia mahitaji ya nchi za kusini katika utandawazi na maendeleo ya baadaye.

    Mikataba kadhaa ya kuunga mkono mkakati wa ushirikiano wa kiuchumi itasainiwa mbele ya viongozi wa nchi za BRICS kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako