• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la viwanda na biashara la BRICS lafunguliwa China

    (GMT+08:00) 2017-09-03 15:53:35

    Kongamano la viwanda na biashara kati ya nchi za BRICS limefunguliwa leo alasiri mjini Xiamen, China. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa kongamano hilo.

    Hili ni kongamano kubwa zaidi tangu mfumo wa BRICS uanzishwe miaka 10 iliyopita, na kuwashirikisha wajumbe zaidi ya 1,000 kutoka nyanja za viwanda na bishara, wakiwemo wakuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, na Benki mpya ya Uendelezaji ya Nchi za BRICS.

    Kongamano hilo litajadili hasa masuala manne ya biashara na uwekezaji, ushirikiano wa kifedha na maendeleo, kuunganishana miundo mbinu, na uchumi wa bahari. Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping amekumbusha historia ya mfumo wa BRICS, na kujumuisha uzoefu wa ushirikiano kati ya nchi wanachama wake, na kutupia macho mustakabali wa mfumo huo. Rais Michel Temer wa Brazil na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pia wamehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa kongamano hilo.

    Takiwmu zinaonesha kuwa hadi sasa thamani ya uchumi wa nchi tano wanachama wa RRICS ni asilimia 23 ya dunia nzima, na nchi hizo zimechangia asilimia 50 ya ongezeko la uchumi wa dunia. Hadi kufikia mwaka 2030, uchumi wa nchi hizo utakuwa mkubwa zaidi kuliko nchi saba za magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako