• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la serikali ya Iraq lawaua wapiganaji zaidi 2,000 wa IS katika vita vya kuikomboa Tal Afar

    (GMT+08:00) 2017-09-03 17:53:03

    Jeshi la Iraq jana limesema kuwa jeshi la serikali liliwaua wapiganaji zaidi 2,000 wa kundi la Islamic State katika operesheni ya kuikomboa Tal Afar, na askari 115 wa jeshi la serikali la Iraq walikufa katika operesheni hiyo.

    Msemaji wa idara ya kamanda ya operesheni ya ushirikiano ya Iraq Bw. Abdul-Amir Yarallah katika taarifa baada ya vita alisema kuwa, chini ya uungaji mkono wa jeshi la anga la serikali na ndege za vita za shirikisho la kupambana na ugaidi la kimataifa, askari zaidi 40,000 wa vikosi mbalimbali tarehe 20 mwezi Agosti walianza operesheni ya kuikomboa Tal Afar ambayo ni kituo muhimu cha mwisho cha kundi la IS kwenye sehemu ya kaskazini ya Iraq, na kuwaua wapiganaji zaidi 2,000 wa kundi la IS katika vita vya siku 12. Aidha, jeshi la serikali lilivunja mahandaki 66, na kugundua viwanda 13 vya kutengeneza mabomu na kukamata silaha na mabomu mengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako