• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa taarifa kuhusu jaribio la silaha ya nyuklia la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-03 17:57:20

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa taarifa kuhusu kufanya tena jaribio la silaha ya nyuklia kwa Korea Kaskazini, ikisema kuwa serikali ya China inakipinga kithabiti na kukilaani vikali kitendo cha Korea Kaskazini.

    Wizara ya mambo ya nje ya China ilisema kuwa kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, kulinda mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia, kulinda amani na utulivu wa Asia ya Kaskazini Mashariki ni msimamo thabiti wa China pia ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa. China inaihimiza Korea Kaskazini isipuuze msimamo wa jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, kutekeleza kihalisi maazimio husika ya baraza la usalama, kusimamisha vitendo vyenye makosa na kurudisha kwenye njia ya kutatua suala kwa mazungumzo ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako