• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Al-shabaab yashambulia kituo cha kijeshi Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-03 18:49:24

    Kundi la Al-Shabaab limeshambulia na kuchukua udhibiti wa kituo cha kijeshi nje ya jiji la Kismayu la pwani ya Somalia. Afisa mwandamizi wa jeshi Ismail Sahardid aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wapiganaji hao walishambulia kituo hicho kaskazini mwa Kasmayu na kufanya mapigano makali na askari wa Somalia.

    Habari zinasema katika mashambulizi hayo, wapiganaji wasiopungua 20 wameuawa.

    Wakati huo huo, polisi nchini Kenya imesema watu wanaohisiwa ni kundi na Al-Shabaab wamewaua maafisa wawili wa polisi wa Kenya baada ya kuharibu kanisa katika kanda ya pwani ya Kwale.

    Kamanda wa polisi wa kikanda Lorrie Kieng alisema wapiganaji waliokuwa wakiendesha pikipiki walivamia kanisa la Anglican nchini humo kabla ya kukimbia na bunduki mbili za maafisa waliouawa waliokuwa wakilinda waumini huko Ukunda.

    maeneo kadhaa kaskazini mwa Kenya ikiwa ni pamoja na mikoa ya pwani kwenye mipaka ya Somalia imekuwa ikilengwa wa wapiganaji wa Al-Shabaab ambao huua wananchi wasiokuwa na hatia, pamoja na maafisa wa usalama na viongozi wengine wa serikali wakitumia bunduki na mabomu ya kujiua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako