• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UEFA yaanza uchunguzi kwa klabu ya PSG juu ya matumizi ya fedha

    (GMT+08:00) 2017-09-04 08:40:56
    Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA limeanza uchunguzi katika klabu ya Paris St German hususani katika kukagua uvunjwaji wa sheria mpya ya Shirikisho hilo ya Klabu kutumia fedha nyingi kuliko kiasi inachoingiza ili kupata mafanikio inayofahamika kama 'UEFA Financial Fair Play Regulation' FFP.

    Hatua hiyo ya Shirikisho inakuja baada ya PSG kufanya usajili ghali duniani wa mchezaji Neymar Jr. kutoka Barcelona kwa ada ya Pauni milioni 220 ada ambayo imeongezeka pauni milioni 100 zaidi ya ile ya Mchezaji ghali msimu 2016-2017 kiungo Paul Pogba huku timu hiyo ikihusishwa pia kutoa zaidi ya Pauni milioni 160 kwa kinda Kylian Mbappe ambaye amejiunga na Klabu hiyo kwa mkopo akitokea Monaco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako