Russia imeitaka Marekani kurudisha mali zake za kidiplomasia zilizozuiwa nchini humo, na kutaja kitendo hicho cha Marekani kama hatua ya uhasama inayokiuka sheria za kimataifa. Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Russia inasema kama Marekani ikikataa kurudisha mali hizo, itawajibika na kushushwa kwa ngazi ya uhusiano kati ya Russia na Marekani, ambao ni msingi muhimu kwa utulivu na usalama wa kimataifa. Kauli hiyo ya Russia imekuja baada ya Marekani kufunga ubalozi mdogo wa Russia mjini San Francisco na ofisi ya mwakilishi wa kibiashara wa Russia mjini Washington Jumamosi iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |