• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Operesheni ya kulisambaratisha kundi IS kuchukua saa kadhaa Deir al-Zour

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:26:24

    Operesheni ya kulisambaratisha kundi la IS linalouzingira mji wa Deir al-Zour inatarajiwa kuchukua saa kadhaa, wakati jeshi likiendelea kusonga mbele kwa kasi kuelekea lilipo kundi IS.

    Jeshi la Syria tayari limeingia kwenye mpaka wa jimbo la Deir al-Zour mashariki mwa Syria, wakati ambapo wapiganaji wa IS wanashambulia mji kwa mizinga, kufuatia raia kusherehekea na kuwasubiri kwa hamu wanajeshi kufika. Jeshi hilo limeshadhibiti maeneo muhimu na kubaki kilomita 10 kabla ya kufika kwa kikosi cha 137 magharibi mwa Deir al-Zour ambako wanajeshi wa Syria wamezingirwa. Mji wa Deir al-Zour umezingirwa na IS tangu mwaka 2015 na kudhibiti eneo kubwa lenye utajiri wa mafuta, karibu na mpaka wa Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako