• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kuandaa mkutano wa kilele wa nchi za BRICS mwakani

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:38:04

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema Afrika Kusini itaandaa mkutano wa kilele wa 10 wa nchi za BRICS mwaka 2018

    Kwenye kongamano la viwanda na biashara la nchi za BRICS lililofunguliwa jana mjini Xiamen, kusini mashariki mwa China, rais Zuma amewakaribisha washiriki hao kuitembelea Afrika Kusini kwenye mkutano huo kwa ajili ya uwekezaji wenye mustakabali mzuri na nafasi nyingi.

    Ameongeza kuwa bara la Afrika ni sehemu mpya yenye mustakabali mkubwa wa ukuaji na ustawi. Amesema Afrika Kusini inataka uchumi wake uwe na maendeleo shirikishi na kuhimiza biashara chini ya ushirikiano na nchi za BRICS. Mwaka jana thamani ya biashara kati ya Afrika Kusini na nchi hizo ilifikia dola za bilioni 31.2 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako