• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yaitaka Israel ifute uamuzi wa kuanzisha tume ya usimamizi wa wakazi wa Wayahudi

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:40:06

    Katibu mkuu wa kamati ya utendaji kwenye Chama cha ukombozi wa Palestina PLO Bw Saeb Erakat, ametoa taarifa ya kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ili kuilazimisha Israel ifute uamuzi wake wa kuanzisha tume ya usimamizi wa wakazi wa Wayahudi mjini Hebron, kwenye ukingo wa magharibi.

    Bw Erakat ameuhimiza Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Russia zichukue hatua za kiutendaji ili kuilazimisha Israel kufuta uamuzi huo.

    Ameongeza kwamba uamuzi huo unahalalisha makazi hayo yaliyoko ardhi ya Palestina inayokaliwa, kitendo ambacho kinakiuka sheria ya kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa.

    Jeshi la Israel limesaini amri siku za karibuni kuamua kuanzisha tume ya usimamizi wa wakazi Wayahudi kwa ajili ya kuwapatia huduma, ambayo inamaanisha kukubali rasmi hadhi halali ya makazi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako