• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laitisha mkutano wa dharura kujadili jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:49:23

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeitisha mkutano wa dharura kujadili majaribio ya bomu la nyuklia ya Korea Kaskazini, kutokana na pendekezo lilitolewa na balozi Nikki Haley wa Marekani na wenzake wa Japan, Ufaransa, Uingereza na Korea Kusini.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw António Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake kulaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini.

    Aidha, rais wa Marekani Donald Trump amesema, anafikiria kusimamisha ushirikiano wote wa kibiashara na nchi zinazofanya biashara na Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako