• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wakutana Xiamen

    (GMT+08:00) 2017-09-04 10:11:52

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Russia Vladmir Putin, ambaye yuko mjini Xiamen, China kuhudhuria mkutano wa 9 wa viongozi wa nchi za BRICS.

    Rais Xi Jinping amesema, kutoka na hali ilivyo sasa, kuimarisha ushirikiano wa nchi za BRICS kunaendana na maslahi ya pamoja ya nchi hizo, pia ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa hasa nchi zenye soko jipya na nchi zinazoendelea. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za BRICS kufanikisha mkutano wa Xiamen, na kutekeleza matokeo yatakayopatikana kwenye mkutano huo.

    Kwa upande wake Rais Putin amesema ni muhimu kwa Russia na China kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu, kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati na kuzidisha mawasiliano katika masuala ya kimataifa na ya kikanda. Amesema Russia inaiunga mkono China kuandaa mkutano wa kilele wa nchi za BRICS na mazungumzo ya nchi zenye soko jipya na nchi zinazoendelea.

    Pia marais hao wamebadilishana maoni kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea, na kukubaliana kuwa kushikilia lengo la kutimiza peninsula ya Korea isiyo na nyuklia, na kutatua kwa njia mwafaka hali mpya baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lingine la nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako