• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Korea Kusini lafanya mazoezi ya kurusha makombora baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-09-04 18:43:37

    Jeshi la Korea Kusini leo limefanya mazoezi ya makombora ikiwa ni siku moja baada ya Kroea Kaskazini kufanya jaribio la sita la silaha ya nyuklia.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na baraza la wanajimu wakuu wa jeshi la Korea Kusini imesema, jeshi la anga na la ardhini lilifanya zoezi la pamoja mapema leo katika pwani ya mashariki nchini humo, na kusema makombora yaliyorushwa na jeshi la ardhini na la anga yalifanikiwa kupiga maeneo yaliyolengwa kwa usahihi.

    Wakati huohuo, mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini Choo Mi-ae amependekeza kupeleka ujumbe maalum nchini Marekani na Korea Kaskazini ili kutatua suala la nyuklia katika peninsula ya Korea. Bi. Choo amekiambia kikao cha bunge la nchi hiyo kuwa serikali haitakiwi kuacha juhudi za majadiliano na inapaswa kupinga aina yoyote ya vita kutokea kwenye peninsula hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako