• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kuunga mkono zaidi maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-04 18:53:59

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma, na kuahidi kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini na kuunga mkono amani na maendeleo barani Afrika.

    Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Afrika Kusini uko katika kipindi kizuri katika historia, na kwamba katika miaka kadhaa iliyopita, nchi hizo zimewekeza nguvu kubwa ya maendeleo katika uhusiano wa kimkakati wa pande zote. Amesema, China iko tayari kuimarisha uratibu na Afrika Kusini na kupanua uhusiano kupitia mafanikio mengi zaidi katika ushirkiano ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Rais Zuma amesema, Afrika Kusini iko tayari kuimarisha ushirikiano na China. Pia amesema, nchi hizo mbili zitaungana mkono katika kuandaa mikutano ya BRICS mwaka huu na ujao, huku akiongeza kuwa uhusiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili ni imara na wenye nguvu kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako