• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi nne za Afrika na mkoa wa Jilin nchini China kuzindua miradi ya ushirikiano

    (GMT+08:00) 2017-09-04 18:54:22

    Semina ya ushirikiano wa kilimo kati ya mkoa wa Jilin, China na nchi nne za Afrika imefanyika huko Changchun, mji mkuu wa mkoa huo, na kuhudhuriwa na viongozi na wajumbe zaidi ya 200 kutoka serikali na mashirika ya China, Uingereza na nchi nne za Afrika ikiwemo Ethiopia, Kenya, Msumbiji na Zambia.

    Semina hiyo iliyoandaliwa na kamati ya kuhimiza biashara ya China, kituo cha kimataifa cha biashara cha Umoja wa Mataifa, serikali ya mkoa wa Jilin na mfuko wa maendeleo wa China na Afrika, inalenga kuanzisha njia ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya makampuni ya nchi nne za Afrika na wawekezaji wa China, ili kuweka msingi kwa ajili ya miradi ya uwekezaji ya kampuni za China katika nchi hizo.

    Kwenye semina hiyo, wataalamu husika kutoka idara zinazohimiza uwekezaji na biashara za nchi nne za Afrika wamejulisha kampuni za China mazingira ya uwekezaji na miradi katika sekta za kilimo katika nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako