• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za BRICS wakubali kukuza uhusiano wa kiwenzi

    (GMT+08:00) 2017-09-04 19:04:48

    Mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi za BRICS umefanyika leo mjini Xiamen, China. Mkutano huo umeendeshwa na rais Xi Jinping wa Chinana umehudhuriwa na wenzake Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Michel Temer wa Brazil, Vladimir Putin wa Russia na waziri mkuu wa India Bw Narendra Modi. Azimio la Xiamen lililopitishwa na mkutano huo limesisitiza kuwa jitihada za pamoja zitafanyika ili kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi wanachama wa BRICS, na kuanzisha mwongo wa pili wenye ushirikiano mzuri.

    Baada ya maendeleo ya miaka 10, nchi tano wanachama wa BRICS zinachangia asilimia 50 ya ongezeko la uchumi wa dunia, na zimekuwa injini ya maendeleo ya uchumi duniani na nguvu muhimu katika mambo ya kimataifa. Katika mkutano wa Xiamen ambao umefanyika wakati muhimu wa kuendeleza ushirikiano wa BRICS, rais Xi kwanza amefanya majumuisho ya uzoefu wa ushirikiano huo katika miaka 10 iliyopita.

    "Sababu ya kuendelezwa kwa kasi kwa ushirikiano kati ya nchi za BRICS ni njia sahihi ya kushirikiana, yaani kuheshimiana na kusaidiana, kufuata njia inayolingana na hali ilivyo nchini, kufuata kanuni ya kufungua mlango, kusikilizana na kushirikiana ili kupata mafanikio ya pamoja, kuhimiza ushirikiano katika sekta za uchumi, siasa na utamaduni, kupendekeza usawa na haki katika mambo ya kimataifa, na kushirikiana na nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea, ili kuanzisha mazingira mazuri ya kimataifa kwa juhudi za pamoja."

    Maoni ya nchi za BRICS yanafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na ongezeko la vitendo vya kupinga mafungamano na kujilinda kibiashara. Rais Xi amezihimiza nchi za BRICS kuongeza ushirikiano halisi na uratibu katika mambo ya kimataifa, na kupendekeza kusukuma mbele ushirikiano wa kiuchumi, kuimarisha na kuendeleza mawasiliano ya mikakati, kuhimiza utaratibu wa kimataifa uwe na usawa na haki zaidi, na kuhamasisha mawasiliano kati ya wananchi wao. Ametangaza kuwa China itatenga yuan milioni 500 sawa na dola za kimarekani milioni 77.5 kwa mpango wa kwanza wa ushirikiano na mawasiliano kati ya nchi za BRICS katika mambo ya uchumi na teknolojia, na dola milioni 4 kwa ajili ya mfuko wa kuazisha benki mpya ya maendeleo. Alipozungumzia juhudi za kuhimiza utaratibu wa kimataifa uwe na usawa na haki zaidi, anasema,

    "Tunatakiwa kujiunga na utawala wa kimataifa, kwani bila ya ushiriki wa nchi zetu, masuala mengi muhimu duniani hayatatuliki. Tunapaswa kutoa sauti na mapendekezo ya pamoja kuhusu masuala ya amani na maendeleo duniani, hali ambayo inafuata matarajio ya jumuiya ya kimataifa, na pia inalingana na maslahi yetu ya pamoja."

    Amezihimiza nchi za BRICS kusukuma mbele mafungamano ya kiuchumi duniani kwa kufuata kanuni ya kufungua mlango, kukubaliana, kunufaisha pande zote, na kuwa na uwiano na mafanikio ya pamoja, na pia kusukuma mbele mageuzi ya utawala wa uchumi duniani, na kuongeza uwakilishi na ushawishi wa nchi zinazoendelea, ili kupunguza pengo kati ya nchi za kusini na kaskazini, na kutia nguvu mpya kwenye maendeleo ya uchumi wa dunia. Katika miaka ya hivi karibuni, mbali na kuongeza ushirikiano wa jadi katika usalama wa uchumi na siasa, nchi za BRICS pia zimeimarisha ushirikiano kati yao katika mambo ya utamaduni, ili kupata nguzo ya tatu. Rais Xi anasema,

    "Tunafurahi kuona makubaliano kati ya viongozi wa nchi za BRICS ya kuhimiza mawasiliano ya utamaduni yanatekelezwa na kuwa hali halisi. Mwaka huu ushirikiano huo utafanywa katika nyanja mbalimbali. Hadi sasa tumefanya michezo ya wanariadha, tamasha la filamu, tamasha la utamaduni, na mkutano kuhusu matibabu ya jadi. Natumai kuwa kutokana na juhudi zetu za pamoja, ushirikiano huo utafanyika mara kwa mara, na kuwashirikisha watu wa kawaida."

    Katika mchakato wa ushirikiano kati ya nchi za BRICS, miaka 10 ni kipindi cha mwanzo tu. Rais Xi amesema China inaamini kuwa ushirikiano huo utapata maendeleo makubwa zaidi katika siku zijazo, na nchi za BRICS zitatoa mchango zaidi katika mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako