• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Mexico

    (GMT+08:00) 2017-09-04 19:07:35

    Rais Xi Jinping wa China huko Xiamen, China amekutana na mwenzake wa Mexico Enrique Peña Nieto ambaye yuko China kuhudhuria mazungumzo ya nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umefungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa pande zote, na kwamba nchi hizo zinadumisha mawasiliano mazuri katika serikali, idara za sheria na majeshi. Amesema pande hizo mbili zimepata maendeleo katika ushirikiano kwenye sekta za mafuta na gesi, mawasiliano ya habari, mambo ya kifedha, nishati safi, utengenezaji na safari za anga.

    Kwa upande wake, Rais Nieto amesema, mazungumzo ya nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea yaliyoandaliwa na China yana umuhimu mkubwa. Amesema kuanzishwa kwa uhusiano wa kimkakati na wenzi wa pande zote kati ya nchi hizo mbili utasukuma mbele biashara na uwekezaji pamoja na mawasliano ya watu. Pia ameongeza kuwa Mexico inapenda kushiriki kwenye pandekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ili kuimarisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali.

    Rais Xi pia amekutana na waziri mkuu wa Thailand, Prayuth Chan-ocha ambaye anahudhuria mikutano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako