• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki ya Equity kupitia mikopo ya simu za mkononi imepanda hadi Sh bilioni 57

    (GMT+08:00) 2017-09-04 20:54:01

    Benki ya Equity kufikia sasa imepeana mkopo wenye thamani ya sh bilioni 57 kupitia jukwaa la Equitel iliyozinduliwa mwezi Mei 2014.

    Benki kubwa ya Kenya kwa namba ya wateja wake imesema jumla ya maombi ya mkopo ni sh milioni 7.5, na nane kati ya kila mkopo inapeanwa kwa njia ya Equitel.

    Mtendaji Mkuu wa Benki hizo James Mwangi amesema urahisi wa kupata mikopo kupitia simu za mkononi umeona Equitel ikiongeza wastani wa mkopo hadi sh 8,200 katika nusu ya mwaka hadi mwezi Juni mwaka 2017 ikilinganishwa na Sh3,900 mwezi Juni 2015.

    Programu za kukopesha mikopo ya benki kupitia njia ya simu za mkononi kama vile M-Shwari, Equitel, M-Co-op Fedha, na KCB M-Pesa zimebadilisha sana, jinsi Wakenya wanavyopata mikopo, kwa vile wateja hawana haja ya kujaza makaratasi marefu, kutoa dhamana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako