• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yatarajia kuwa nguzo mpya ya ukuaji kupitia ushirikiano na BRICS

    (GMT+08:00) 2017-09-05 09:35:34

    Viongozi wa Afrika wamesema kuwa bara hilo linatarajia kuwa nguzo mpya ya ukuaji kupitia ushirikiano na nchi za Brazil, Russia, India, China, na Afrika Kusini, zinazounda kundi la BRICS.

    Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa biashara wa BRICS uliofanyika jumapili mjini Xiamen, China, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alisema kuwa anatarajia nchi za BRICS zinaweza kuboresha ushirikiano ili kufanya uchumi wao kuwa mkubwa na endelevu, hivyo kuwanufaisha wananchi wao nchi hizo. Naye rais al-Sisi wa Misri amesema, nchi yake imetunga sera mfululizo za mageuzi katika mfumo wa ruzuku, usalama wa jamii na mambo ya fedha, pia imeboresha mazingira ya uwekezaji na biashara.

    Akizungumza kwenye Mjadala wa Masoko yanayoibuka na Nchi Zinazoendelea, rais Alpha Conde wa Guinea, ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, amesema maendeleo ya ushirikiano wa BRICS yameleta matumaini kwa nchi zote zilizo nyuma kimaendeleo duniani, na kuongeza kuwa anatarajia uhusiano kati ya Guinea na nchi za BRICS utaifanya Afrika kuwa na sura mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako