• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yakanusha kauli ya mauaji ya raia wa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-05 09:56:05

    Serikali ya Afrika Kusini imekanusha madai kuwa raia wa wageni nchini humo, hususan kutoka Somalia wanauawa mjini Cape Town.

    Waziri katika ofisi ya rais nchini Afrika Kusini Bw Jeff Radebe amesema madai ya kuwatenga raia wa Somalia kuwa waathirika wa uhalifu siyo sahihi. Radebe amesema kuwa uhalifu unaathiri kila mtu bila kujali uraia na kabila, na kwamba aina hiyo ya utengano itasababisha unyanyapaa kwenye jamii na kuchochea mapambano dhidi ya makundi mengine. Jumuiya ya Wasomali nchini Afrika Kusini SCBSA imedai kuwa, tangu mwanzo wa mwaka huu, makumi ya wakimbizi wa Somalia wameuawa nchini Afrika Kusini, hususan katika eneo la makazi duni la Khayelitsha mjini Cape Town.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako