• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wachambua mapendekezo ya rais wa China kuhusu ushirikiano kati ya nchi za BRICS

    (GMT+08:00) 2017-09-05 10:10:15

    Mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi za BRICS ulifanyika jana mjini Xiamen, China, ambapo hotuba aliyoitoa rais Xi Jinping wa China na Azimio la Xiamen lililopitishwa kwenye mkutano huo zinafuatiliwa sana duniani.

    Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bw. Guo Xiangang anaona kuwa, ushirikiano wenye ufanisi katika sekta ya uchumi ni msukumo muhimu wa kuhimiza maendeleo ya kasi ya nchi za BRICS katika miaka kumi iliyopita, na ushirikiano kama huo unapaswa kuimarishwa katika miaka 10 ijayo.

    Ushirikiano huo pia ni sehemu muhimu katika Azimio la Xiamen. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa mambo ya fedha ya Chongyang katika Chuo Kikuu cha Umma cha China Bw. Wang Wen akizungumzia azimio hilo anasema:

    "Uwezo wa nchi za BRICS bado haujaendelezwa kikamilifu, haswa katika sekta ya uwekezaji wa biashara. Hivi sasa biashara na uwekezaji kati ya nchi za BRICS bado ni mdogo, kiasi ambacho kinachukua asilimia 16.6 na asilimia 6 tu mtawalia ililinganishwa na biashara na uwekezaji wa jumla wa nchi hizo tano. Takwimu hiyo haiendani kabisa na hali ya BRICS ambayo inachukua asilimia 25 ya thamani ya jumla ya uchumi wa dunia, na yenye karibu nusu ya jumla ya watu duniani. Nchi za BRICS zitaweza kupata maendeleo makubwa zaidi iwapo ushirikiano wa kiuchumi kati yao utakuzwa kwa kina zaidi."

    Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bw. Guo Xiangang anasema:

    "BRICS ulikuwa ni utaratibu uliokuwa unatoa kipaumbele ushirikiano wa kiuchumi. Katika mkutano huu rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la kuanzisha ushirikiano katika sekta ya usalama katika miaka 10 ijayo. Naona pendekezo hili ni muhimu sana, kwa kuwa maendeleo ya uchumi hayawezi kupatikana bila ya mazingira salama. Kwa hiyo nchi za BRICS zinahitaji kuzingatia amani na utulivu wa kikanda na dunia katika muongo wake wa pili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako