• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi kupokea wakimbizi elfu 15 wanaorudi kutoka Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-09-05 10:16:03

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Terence Ntahiraja amesema, nchi hiyo inapanga kupokea wakimbizi zaidi ya elfu 15 wanaorudi makwao wakitokea Tanzania wiki hii.

    Bw. Ntahiraja amesema, mkutano kuhusu kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ulifanyika tarehe 31 mwezi uliopita, ambapo wajumbe kutoka Burundi, Tanzania, na UNHCR waliamua awamu ya kwanza ya wakimbizi zaidi ya elfu 15 walioko nchini Tanzania wanatakiwa kurudi Burundi jumanne wiki hii kupitia mpaka wa mkoa wa Makamba, kusini mwa Burundi.

    UNHCR itatoa chakula na vitu vingine kwa wakimbizi waliorudi kwa kipindi cha miezi mitatu wakati wanapojiunga tena kwenye jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako