• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS wafungwa

    (GMT+08:00) 2017-09-05 18:19:49

    Mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS umemalizika leo mjini Xiamen, China. Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rais Xi Jinping wa China amesema, kwenye mkutano huo viongozi wa nchi za BRICS wamesisitiza umuhimu wa moyo wa BRICS wa kufungua mlango, kukubaliana, kushirikiana na kupatia mafanikio ya pamoja, na kutunga mpango mpya kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano halisi katika sekta mbalimbali. Nchi za BRICS zimeamua kuchukua mkutano wa Xiamen kuwa mwanzo mpya, kujenga uhusiano wa wenzi wa kimkakati wenye mshikamano, mpana na kamilifu zaidi, na kuanzisha mwongo wa pili wa ushirikiano mzuri.

    Kauli mbiu ya mkutano huo ni kukuza uhusiano wa wenzi kati ya nchi za BRICS, na kuanzisha mustakabali mzuri zaidi. Kwa kufuata kauli mbinu hiyo, viongozi wa nchi wanachama wa BRICS wamebadilishana maoni kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo, kufanya mawasiliano ya utamaduni, kusukuma mbele ujenzi wa mfumo na kushiriki kwenye utawala wa uchumi wa dunia. Rais Xi anasema,

    "Mkutano huu ulipitisha Azimio la Xiamen la Viongozi wa Nchi za BRICS, ambalo limesisitiza moyo wa BRICS wa kufungua mlango, kushirikiana na kupatia mafanikio ya pamoja, kujumuisha uzoefu wa mafanikio ya ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika miaka 10 iliyopita, na kutunga mpango mpya wa kukuza zaidi uhusiano wa wenzi na ushirikiano kati ya nchi hizo katika sekta mbalimbali."

    Hivi sasa, hali ya dunia imekuwa na mabadiliko makubwa yenye utata, na nchi za BRICS pia zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi, hivyo ni muhimu sana kwa nchi hizo kuongeza ushirikiano. Rais Xi ameeleza kuwa, nchi hizo zinapaswa kuongeza mawasiliano na uratibu katika mambo muhimu, kulinda kanuni za uhusiano wa kimataifa, kushirikiana ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimataifa, na kuharakisha mageuzi ya utawala wa uchumi wa dunia. Pia amezihimiza nchi hizo kuongeza ushirikiano mbalimbali, hasa katika masuala ya usalama wa kisiasa ili kuongeza uaminifu wa kimkakati, na kufanya mawasiliano ya utamaduni mara kwa mara ili kuongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wao.

    Rais Xi amesema, wakati ushirikiano wa mfumo wa BRICS unapoingia mwongo wa pili, ujenzi wa mfumo huo unapaswa kuendelezwa bila ya kusita, ili kutoa uungaji mkono imara kwa ajili ya kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi wanachama wake. Alipozungumzia namna ya kuimarisha ujenzi wa mfumo huo, rais Xi anasema,

    "Sisi Sote tumekubali kuimarisha kazi ya uratibu, ili kuchunguza hali ya utekelezaji wa makubaliano ya mikutano kila baada ya kipindi fulani. Tunatafuta njia mpya ya kufanya ushirikiano ili kushikamana zaidi. Mwaka huu, ujenzi wa mfumo wa BRICS umepiga hatua mpya, licha ya kuanzisha utaratibu wa kufanya mkutano rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje na mkutano wa wajumbe wetu katika Umoja wa Mataifa kila baada ya muda, pia tumehamasisha kujenga mtandao wa forodha ya kielektroniki, kikundi cha watu wanaoshughulikia biashara ya kielektroniki, jumuiya ya majumba ya makumbusho, jumuiya ya majumba ya michoro na jumuiya ya maktaba. Hivi vitatoa uungaji mkono imara kwa ajili ya kukuza ushirikiano kati yetu katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni."

    Kufanya mazungumzo na ushirikiano na nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea ni desturi ya mfumo wa BRICS. Ukiwa tofauti na mikutano mingine, mkutano huo ulihudhuriwa na nchi nyigine zisizo wanachama wa BRICS. Rais Xi anasema,

    "Viongozi kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wanakubali kuwa, nchi zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea zina mwelekeo mzuri wa kujiendeleza kiuchumi, na zinapaswa kuchangia zaidi juhudi za kimataifa za kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na kukamilisha utawala wa uchumi wa dunia. Zitakuza ushirikiano kati ya nchi za kusini, na kujenga mfumo mpya wa BRICS unaoshirikisha nchi nyingi zaidi, ili kutafuta njia mpya ya kutimiza maendeleo endelevu, na kutoa mchango zaidi kwa ongezeko la uchumi wa dunia, na maendeleo ya pamoja ya nchi zote duniani."

    Mkutano wa kumi wa viongozi wa nchi za BRICS utafanyika mwaka ujao mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Xi ameahidi kuwa China itashirikiana na pande nyingine kuunga mkono mkutano huo, ili kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa BRICS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako