• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Misri

    (GMT+08:00) 2017-09-05 18:36:39

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi huko Xiamen, China

    Rais Xi amemkaribisha rais al-Sisi kwenye mazungumzo ya nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea, na kusema katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Misri unaendelezwa kwa kasi, miradi mikubwa ya ushirikiano inaendelea kutekelezwa, na maendeleo yamepatikana katika mawasiliano ya utamaduni.

    Amesema China inataendelea kuiunga mkono juhudi za Misri za kulinda utulivu na kuharakisha ukuaji, na kushirikiana nayo katika maendeleo na mageuzi na njia ya kutimiza ustawi wa taifa.

    Rais al-Sisi amesema, Misri inatilia maanani uhusiano kati yake na China, na inaridhishwa na maendeleo ya uhusiano huo. Pia itaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kupenda kuunganisha mikakati yake ya kujiendeleza na pendekezo hilo, ili kuzidisha ushirikiano na China katika uwekezaji na miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako