• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenzake wa Guinea

    (GMT+08:00) 2017-09-05 18:36:59

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Guinea Alpha Condé ambaye yuko ziarani nchini China na kuhudhuria mazungumzo ya nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea.

    Rais Xi amesema, tangu uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China na Guinea uanzishwe mwaka mmoja uliopita, ushirikiano huo umeonesha mwelekeo mzuri wa maendeleo. Amesema China inatilia maanani uhusiano kati yake na Guinea na kupenda kushirikiana na nchi hiyo kuhimiza uhusiano huo ili kuwanufanisha watu nchi hizo mbili. Amesema katika kipindi kijacho, pande mbili zitaimarisha uaminifu wa kisiasa, na kuungana mkono katika maslahi kuu na masuala muhimu yanayofuatiliwa.

    Rais Condé amemshukuru rais Xi kwa kumwalika kuhudhuria mazungumzo hayo akiwa mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, huku akisema hatua hiyo imeonesha kuwa China inaitilia maanani Afrika. Pia amesema, Guinea inapenda kushirikiana na China katika sekta za uvuvi na madini na shughuli za maendeleo ya Afrika Magharibi na kuimarisha mawasiliano ya utawala wa kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako