• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping amwambia waziri mkuu wa India kuwa nchi zao zinahitaji kuwa na uhusiano mzuri na imara

  (GMT+08:00) 2017-09-05 18:39:38

  Rais Xi Jinping wa China amesema uhusiano mzuri na tulivu kati ya China na India unaendana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili.

  Rais Xi amesema China iko tayari kufanya kazi na India kwa msingi wa kanuni tano za kuishi kwa pamoja kwa masikilizano ili kuboresha kuaminiana, kunufaishana na kufanya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili uwe kwenye njia nzuri.

  Rais Xi amesema hayo alipokutana na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi kwenye mkutano wa nchi za BRICS uliofanyika Xiamen, Kusini mwa China.

  Bw. Modi amempongeza Rais Xi Jinping kwa maandalizi mazuri ya mkutano wa nchi za BRICS, na kusema dunia inabadilika kwa kasi na nchi za BRICS zinatakiwa kuimarisha uhusiano wao katika mazingira ya sasa, na kusema mkutano wa BRICS umetoa mchango kwenye lengo hilo.

  Mazungumzo ya viongozi yamefanyika miezi miwili baada ya wanajeshi zaidi ya 270 wa India kuingia kwenye ardhi ya China kuzuia ujenzi wa miundo mbinu, lakini baadaye iliondoa wanajeshi wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako