• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda inahitaji ardhi zaidi kwa ujenzi wa bomba la mafuta

    (GMT+08:00) 2017-09-05 19:26:42

    Serikali ya Uganda imesema inataka ardhi zaidi kwa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima kwenda bandari ya Tanga nchini Tanzania.

    Awali serikali na makampuni yanayoshiriki ujenzi wa bomba hilo walikuwa wamesema wanahitaji ukanda wa mita 30 lakini sasa wanahitaji mita 133 kwa bomba hilo ambalo ndani ya Uganda lina urefu wa kilomita 296.

    Waziri wa ardhi Betty Amongi amesema kipande hicho cha ziada ni cha kujenga miundo mbinu husika kama vile nyaya za umeme, barabara na kutandaza kebo za intaneti.

    Mradi huo wa bomba wa pamoja unatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 ya mafuta kila siku kutoka eneo la ziwa Albert nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako