• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wa mboga, matunda na maua wavuna zaidi soko la Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-09-05 19:31:53

    Wakulima wa mboga, matunda na maua nchini Kenya walipata shilingi bilioni 64 baada ya kuuza bidhaa zao katika soko la ulaya katika kipindi cha miezi 6 ya kwanza ya mwaka 2017 ikilinganishwa na shilingi bilioni 58 kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Kulingana na mamlaka ya chakula na kilimo, maua yalikuwa na ongezeko la asilimia 23 huku wadau wakiuza tani 85.

    Taakwimu zilizotolewa na serikali zinaonyesha pia wakulima wa matunda wameuza tani 37 za thamani ya shilingi bilioni 5.3 kwenye soko la Ulaya.

    Hata hivyo licha ya kuongezeka kwa mauzo ya mboga wakulima walipata shilingi bilioni 10.8 kutoka kwa tani 42 ikilinganishwa na shilingi bilioni 12.7 za tani 35 mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako