• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda kuanzisha mradi wa kuongeza ubora wa bidhaa

    (GMT+08:00) 2017-09-05 19:32:53

    Halmashauri ya ubora wa bidhaa nchini Rwanda imeanzisha mpango wa kukuza dhamani na ubora wa bidhaa za ndani ya nchi.

    Mpango huo wa miaka 3 kwa jina 'Zamukana Ubuziranenge' unalenga viwanda vidogo na vile vya wastani.

    Chini ya mpango huo viwanda vidogo vitapewa mafunzo kuhusu uwekaji wa viwango na uhakiki wa ubora ili kuzifanya bidhaa zao kushindana zaidi kwenye soko la ndani na la kikanda.

    Mkurungezi wa halmashauri Raymond Murenzi, amesema mradi huo hasa ni wa kukuza biashara zinazoendeshwa na wanawake, vijana na walemavu.

    Murenzi amesema serikali itawekeza frac bilioni 2 kwanza kufanya utafiti wa mradi huo huku tayari frac milioni 300 zikiwa zimetengwa kwa mpango wenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako