• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wenye malori wajiunga kusaidia ujenzi wa nyumba za waalimu Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-09-05 19:33:12

    Chama cha Wamiliki wa Malori ya Kubeba Mchanga Nchini Tanzania (TTOA) kimetoa magari kwa ajili ya kusaidia kubeba mchanga kwa wa ujenzi wa ofisi 402 za walimu Mkoa wa Dar es Salaam.

    Utoaji wa malori hayo umekuja ikiwa ni siku ya tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuomba wadau kujitokeza kuchangia ujenzi wa ofisi hizo lengo likiwa ni kuboresha elimu ya msingi na sekondari katika mkoa huo.

    Akizungumza katika mkutano na Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa Chama hicho, Emmanuel Mushi alisema wamefikia uamuzi huo kama chama ili kuunga mkono jitihada za Makonda na serikali ya kuboresha mazingira katika sekta ya elimu.

    Makonda aliwashukuru kwa msaada huo na kusema kuwa umekuwa wakati muafaka wakati serikali ya mkoa huo ikijipanga kuboresha mazingira mazuri kwa ajili ya walimu katika mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako