• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Acacia yasema ina matumaini ya kusuluhisha mzozo kuhusu mauzo ya mchanga

    (GMT+08:00) 2017-09-05 19:33:45

    Kampuni ya madini ya Acacia imesema ina matumaini kuwa mazungumzo baina yake na Serikali kuhusu kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini nje, yatafikia suluhisho, lakini imetangaza kupunguza uchimbaji madini katika mgodi wake tegemeo wa Bulyanhulu.

    Tangu kuzuiwa kusafirisha mchanga huo mwezi Machi, kampuni hiyo imekuwa ikilalamika kuwa inapoteza mapato, yapatayo dola 1 milioni za Kimarekani (zaidi ya Sh2.2 bilioni) kila siku na sasa hali inaonekana kuwa mbaya zaidi.

    Acacia imesema kuwa imepoteza dola 265 milioni (zaidi ya Sh583 bilioni) ambazo ni sawa na asilimia 35 ya mapato yake tangu mwezi Machi wakati Serikali ilipotangaza kuzuia usafirishaji wa mchanga huo ambao una mabaki ya madini, hasa dhahabu na shaba iliyoshindikana kuchenjuliwa mgodini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako