• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kushiriki kwenye mkutano wa tatu wa kilele wa Umoja wa Afrika kuhusu suala la Libya

    (GMT+08:00) 2017-09-06 09:12:14

    Sudan inatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa tatu wa kilele wa Umoja wa Afrika kuhusu suala la Libya wikiendi hii. Makamu wa rais wa Sudan Bw. Mohamed Abdul-Rahman anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Septemba 9 huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Mkutano huo unalenga kutafuta njia za kuondoa mvutano wa kisiasa unaokwamisha utekelezaji wa makubaliano ya Skhirat yaliyodhaminiwa na Umoja wa mataifa mwaka 2015, na pia utajaribu kuhimiza juhudi za maafikiano ya kitaifa chini ya mapendekezo ya Umoja wa Afrika, jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako