• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tishio la nyuklia, misukosuko ya kibinadamu na mabadiliko ya hewa ni majanga mabaya zaidi duniani

    (GMT+08:00) 2017-09-06 09:30:32

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres jana aliongelea masuala matatu ikiwemo kulaani Korea Kaskazini kwa jaribio lake la nyuklia, mgogoro wa kidini wa Myanmar na kutoa wito wa kuwa makini na mabadiliko ya hali ya hewa baada ya majanga makubwa yanayoikabili dunia.

    Akiongea na wanahabari kuhusu suala la peninsula ya Korea Bw. Guterres ametaka kutumika kwa njia ya mazungumzo na kusisitiza mawasiliano ni muhimu ili kuepuka makosa na kuelewana vibaya, ambayo yanaweza kuleta matokeo yasiyotarajiwa. Kwa upande wa shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa Rohingya huko Myanmar Bw. Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na usalama na haki za binadamu za watu wa jimbo la Rakhine, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kujitahidi kuzuia hali hiyo.

    Na kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, Bw. Guterres amesema umoja wa mataifa uko tayari kuunga mkono juhudi za misaada kwa watu wote wanaosumbuka na majanga ya asili na kusisitiza kuwa sasa ni wakati wa kujenga ujasiri na kupunguza hatari za majanga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako