• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam waishauri Sudan Kusini kuahirisha uchaguzi uliopangwa

    (GMT+08:00) 2017-09-06 09:31:28

    Wataalam na jumuiya za kiraia nchini Sudan Kusini, wameishauri serikali kuahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mapema mwaka kesho, na badala yake kujikita kwenye utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa mwezi Agosti mwaka 2015, ili kukomesha vita iliyodumu kwa miaka mitatu.

    Mtandao wa demokrasia na uchaguzi unaohusisha jumuiya za kiraia zaidi ya 70, umesema hali ya sasa inafanya uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kuaminika uwe mdogo, wakati muda wa utekelezaji wa makubaliano ya amani unatarajiwa kwisha mwezi Agosti mwaka kesho.

    Kutokana na mazingira ya kukosekana kwa usalama, ni wazi kuwa ni vigumu kwa tume ya uchaguzi, vyama vya siasa, jumuiya za kiraia na hata wagombea kufanya shughuli za kisiasa kwa ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako