• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Palestina asema suala la makazi ya Wayahudi ni tishio kwa amani

    (GMT+08:00) 2017-09-06 09:44:02

    Rais Mahamoud Abbas wa Palestina amesema kitendo cha Israel kuendelea na ujenzi wa makazi ya Wayahudi kinatoa tishio kubwa kwa amani kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.

    Rais Abbas alisema hayo jana mjini Ramallah alipokutana na mwenyekiti wa Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu Bw Peter Maurer ambaye yuko ziarani nchini Palestina.

    Akizungumza na wanahabari kuhusu mkutano wao, Ofisa wa Ikulu ya Palestina amesema rais Abbas amemjulisha Bw Maurer hali ya sasa ya Palestina na mateso yanayowakabili watu wa Palestina wanaokaliwa na Israel.

    Bw Peter Maurer alitembelea Ukanda wa Gaza mapema jana, na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Kundi la Hamas. Alipokutana na wanahabari, Bw Maurer amesema mazungumzo hayo yanahusu msukosuko wa kibinadamu unaowakabili watu wa Ukanda wa Gaza. Amesisitiza kuwa Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu itaendelea kutoa msaada kwa watu wa Gaza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako