• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania kutumia vyandarua vya dawa kupambana na malaria

  (GMT+08:00) 2017-09-06 09:51:41

  Tanzania itasambaza vyandarua vya dawa milioni 28 vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni 28, ili kupambana na malaria.

  Mkuu wa matibabu ya malaria katika Wizara ya Afya ya Tanzania Bw. Sixbert Mkude amesema hivi sasa malaria ni moja ya magonjwa matano yanayosababisha vifo vingi nchini humo. Mwaka huu mikoa kadhaa zikiwemo Geita, Kagera, Mwanza, Tabora, Mara, na Kigoma itapewa kipaumbele kwenye kupambana na ugonjwa huo. Ofisa huyo amesema mbali na kutoa vyandarua, serikali pia itaanzisha kampeni ya kunyunyizia dawa ya kuua wadudu nchini kote.

  Hivi sasa kiwango cha maambukizi ya Mararia nchini Tanzania ni asilimia 14.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako