• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 1,200 wakimbia maeneo yanayodhibitiwa na IS Iraq

    (GMT+08:00) 2017-09-06 10:04:30

    Watu 1,200 wamekimbilia katika mji mmoja unaodhibitiwa na serikali ya Iraq mkoani Anbar magharibi mwa Iraq, kutoka kwenye maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa kundi la IS karibu na mpaka na Syria.

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Anbar Adel al-Dulaimi amesema, serikali ya mji wa Rutba imepokea watu 1,200, wengi wakiwa ni wanawake na watoto, waliokimbia miji ya Aana, Rawa na al-Qaim inayodhibitiwa na wapiganaji wa IS.

    Amesema karibu kila siku serikali ya Iraq inapokea wakimbizi wengi wanaokimbia maeneo yanayodhibitiwa na IS, baadhi yao wanalamizika kulipa pesa nyingi ili kuweza kuondoka maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako