• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Kenya yatoa donge nono la dola laki 1.6 kwa habari kuhusu watuhumiwa wa ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-09-06 10:13:35
    Serikali ya Kenya imetangaza donge nono lenye thamani ya dola za Marekani laki 1.6 kwa wale wanaoweza kutoa taarifa kuhusu watuhumiwa 8 wa ugaidi nchini humo.

    Polisi wamesema donge nono la dola elfu 20 kwa taarifa za kupatikana kwa kila mmoja wa wapiganaji hao limetengwa, ili kuwasaka wapiganaji hao ambao wamekuwa wakifanya operesheni zao kutoka kwenye msitu wa Boni.

    Polisi wamesema kiongozi wa tawi la Kenya la kundi la Al-Shabaab Ahmed Iman Ali pamoja na wapiganaji wengine wanataka kujitoa kutoka kundi hilo baada ya kutoridhika na utendaji wake na sasa wanahofia usalama wao. Uamuzi huo unaonekana kuwavunja moyo wapiganaji wageni wa kundi hilo ambao wanatoka Tanzania, Uganda, Misri na Libya, na kuchochea hali ya wasiwasi kati ya wapiganaji wenyeji na wageni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako